1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

28 waangamia baada ya kituo cha mafuta kushambuliwa Sudan

8 Desemba 2024

Mtandao wa Sudan wa kundi la waokoaji limesema raia 28 wamekufa na wengine 37 wamejeruhiwa wakati kituo cha mafuta mjini Khartoum kiliposhambuliwa. Waliojeruhiwa wanajumuisha watu 29waliochomeka vibaya.

https://p.dw.com/p/4ntME
Sudan |
Vita vya Sudan vyaendelea kuwaangamiza wengi huku mamilioni ya wengine wakiachwa bila makaaziPicha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Mtandao huo pia umetahadharisha kwamba idadi ya waliojeruhiwa huenda ikazidi kupanda. 

Jeshi la Sudan linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan ambalo limekuwa likipambana na wapiganaji wa wanamgambo la RSF wanaoongozwa na Mohammed Hamdan Dagalo tangu mwezi Aprili wamekuwa wakisonga mbele kuingia mjini humo katika wiki za hivi karibuni kwa lengo la kuudhibiti mji huo. 

Mashambulio ya RSF yauwa watu wawili katika kambi ya wakimbizi Darfur

Tangu kuanza kwa machafuko ya Sudan, maelfu ya watu wameuawa huku raia milioni 11 wakipoteza makaazi yao na kusababisha moja ya mgogoro mbaya zaidi wa kibinaadamu kuwahi kushuhudiwa duniani. Hiyo ni kulingana na Umoja wa Mataifa.