1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Watu 515 wamejeruhiwa ajali ya treni za mwendokasi China

15 Desemba 2023

Watu 515, wakiwemo 102 waliopata majeraha mabaya wamepelekwa hospitali nchini China baada ya treni mbili za chini ya ardhi kugongana katika mji mkuu wa Beijing uliokumbwa na theluji hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4aBij
China | Treni za mwendokasi
China inasifika kwa kuwa na mtandao mkubwa wa treni ziendazo kasi na ajali ni jambo la nadra hasa miaka ya karibuni.Picha: CFOTO/NurPhoto/IMAGO

Ajali hiyo imetokea jana jioni katika eneo la milima la magharibi mwa Beijing kwenye njia ya reli ya Changping.

Manispaa ya Beijing imeeleza kuwa, timu ya waokoaji kutoka idara ya zima moto na polisi ilifika katika eneo la tukio na kwamba abiria wote waliokuwemo ndani ya treni hizo wameokolewa.

Theluji nyingi imemwagika katika mji mkuu Beijing tangu siku ya Jumatano, huku shughuli za uchukuzi na masomo zikiathirika. Mamlaka imeuweka mji huo katika tahadhari kutokana na kukumbwa na theluji na baridi kali.