JamiiUrusi
Zaidi ya watu 60 wauawa kwenye tamasha la muziki Moscow
23 Machi 2024Matangazo
Watoto watano wameripotiwa kuwa miongoni mwa majeruhi waliopelekwa hospitali.
Takriban washambuliaji watano waliokuwa wameficha nyuso zao walifyatua risasi kwa watu waliokuwa wakihudhuria tamasha lililofanyika kwenye ukumbi wa Crocus, katika kitongoji cha kaskazini magharibi cha Krasnogorsk.
Soma pia: Kremlin kwa mara ya kwanza yaitaja operesheni ya Ukraine kuwa vita
Ukumbi huo wa Crocus wenye uwezo wa kubeba watu 6,200 ulikuwa unaanda tamasha la muziki wa Rock.
Shambulio hilo linatajwa kuwa moja ya mashambulizi mabaya zaidi nchini Urusi tangu kuvamiwa kwa shule ya Beslan mnamo mwaka 2004 ambapo zaidi ya watu 330, nusu kati yao wakiwa watoto, waliuawa.