1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu saba wakamatwa Ujerumani wakihusishwa na "IS"

31 Mei 2023

Waendesha mashtaka wa Ujerumani wamewakamata watu saba wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS.

https://p.dw.com/p/4S0MU
Deutschland | Symbolbild Polizeieinsatz
Picha: Bjoern Trotzki/IMAGO

Wakati huo huo, polisi wamefanya misako 19 katika majimbo ya Baden-Wuerttemberg, Bremen, Hamburg, Hesse, North Rhine-Westphalia na Rhineland-Palatinate, pamoja na eneo moja nchini Uholanzi. Washukiwa hao wamekamatwa kwa tuhuma za kukusanya michango na kuipeleka kwa IS. Waliokamatwa wanatarajiwa kufikishwa leo na kesho mbele ya mahakama kuangalia iwapo wanapaswa kubakia kizuizini kabla ya kesi yao kusikilizwa. Fedha hizo zilikusanywa kupitia kampeni za kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na majina kama vile ''Dada Yako Kambini,'' ambazo zimekuwa zikiendeshwa kwa miaka kadhaa.