1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu sita wafariki kutokana na kimbunga Oscar huko Cuba

22 Oktoba 2024

Rais Miguel Díaz-Canel ametangaza kwenye televisheni ya taifa kuwa takriban watu 6 wamekufa baada ya kimbunga Oscar kupiga eneo la kisiwa mashariki mwa Cuba kwa usiku wa 4 mfululizo na kusababisha giza katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4m4zd
Kimbunga Oscar katika pwani ya Cuba
Muonekano wa maeneo ya Cuba kutoka kwa Kimbunga Oscar, ikikabiliana na kukatika kwa umeme karibu nchi nzima katika siku yake ya tatu.Picha: NOAA/Handout/AFP

Uharibifu mkubwa umefanyika katika eno la Guantanamo ambalo limefurikwa kwa maji na kusababisha waokoaji kushindwa kufika kutoa msaada wa uokozi. Mamlaka zimesema karibu nyumba 1,000 zimeharibiwa. Kimbunga Oscar kimesababisha kukatika kwa umeme ambapo karibu watu milioni kumi wako gizani tangu siku ya ijumaa, Rais Díaz-Canel amesema mpaka sasa ni theluthi moja tu watu wanapata huduma hiyo kwa sasa. Rais Diaz amesema hatahudhuria tena mkutano wa kilele wa BRICS kutokana na dhoruba hiyo iliyoikumba nchi hiyo.Kimbunga hicho kinaendelea kusababisha mvua kubwa katika maeneo ya masharaiki mwa Cuba na kusini mwa visowa vya Bahamas.