1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wahamishwa kufuatia shambulizi kusini mwa Ukraine

6 Juni 2023

Mamia ya watu wamehamishwa kutoka makaazi yao kwenye eneo la kusini la mto wa Dnipro nchini Ukraine baada ya maji mengi kumwagika kutoka bwawa lililoripuliwa.

https://p.dw.com/p/4SGdq
Ukraine: Kachowka Staudamm schwer beschädigt
Picha: Oleksandr Vlasov via REUTERS

Mamia ya watu wamehamishwa kutoka makaazi yao kwenye eneo la kusini la mto wa Dnipro nchini Ukraine baada ya maji mengi kumwagika kutoka bwawa lililoripuliwa la Nova Kakhovka, na kuzifunika barabara na maeneo ya mji. Urusi inadhibiti ukingo wa kushoto wa mto huo wa Dnipro na bwawa lenyewe, na Ukraine inaudhibiti ukingo wa kulia. Kila upande umemlaumu mwenzake kwa kusababisha uharibifu huo ambao umezusha mzozo wa karibuni katika vita hivyo. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amevilaumu vikosi vya Urusi kwa kufanya shambulizi hilo alilolinganisha na matumizi ya silaha za maangamizi

Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu ameituhumu Ukraine kwa kulilipua bwawa hilo kama sehemu ya mpango wa kuvipeleka vikosi vya askari kutoka mkoa ulio karibu wa Kherson kwa ajili ya operesheni dhidi ya askari wa Urusi.