1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPapua New Guinea

Watu wahamishwa kutoka maeneo hatari Papua New Guinea

28 Mei 2024

Maelfu ya watu wanaoishi karibu na eneo kulikotokea maporomoko ya udongo nchini Papua New Guinea wametakiwa kuhama mara moja kwa sababu ya hatari ya kutokea tena maporomoko hayo.

https://p.dw.com/p/4gN0e
Maelfu ya watu wahamishwa kufuatia tishio la kutokea maporomoko ya udongo
Maelfu ya watu wahamishwa kufuatia tishio la kutokea maporomoko ya udongoPicha: Mohamud Omer/AP/picture alliance

Afisa wa serikali wa mkoa wa Enga kulikotokea mkasa huo, Sandis Tsaka, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, wanafanya kila wawezalo kuwahamisha watu na kwamba sehemu hiyo ni kama "bomu linalosubiri kuripuka."

Afisa huyo ameeleza kuwa idadi ya watu wanaokadiriwa kuathirika na janga hilo ni takriban 7,900.

Mapema siku ya Ijumaa, watu waliokuwa wakiishi sehemu za milimani katika mkoa wa Enga nusra waangamizwe wote baada ya kutokea maporomoko ya udongo katika Mlima Mungalo.

Kituo cha kitaifa kinachoshughulikia majanga kinahofia kuwa zaidi ya watu 2,000 wamezikwa wakiwa hai japo miili ya watu watano tu na mguu wa mwathirika mmoja ndio imetolewa kutoka kwenye udongo hadi sasa.