1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Watu waliokufa kutokana na kimbunga Ufilipino yafikia 388

27 Desemba 2021

Serikali ya Ufilipino imesema idadi ya waliokufa kutokana na kimbunga kikali kilichoikumba nchi hiyo imeongezeka na kufikia watu 388 huku baadhi ya maeneo yalioathirika yakikabiliwa na tishio la kuzuka kwa magonjwa.

https://p.dw.com/p/44rZv
Philippinen Zerstörung nach Rai
Picha: Ferdinandh Cabrera/AFP

Wakati serikali ikishughulika kupeleka chakula, maji na nguo katika maeneo yalioathirika, kitisho kipya kimejitokeza  katika siku za hivi karibuni huku watu 140 wakiugua kutokana na kutumia maji machafu.

Waziri wa afya Maria Rosario Vergeire amesema kuwa watu 80 waliugua ugonjwa wa tumbo katika mkoa wa kusini wa Visiwa vya Dinagat, huku watu 54 wakipatiwa matibabu ya kuharisha hospitalini katika kisiwa jirani cha kitalii cha Siargao

Vergeire amesema kimbunga hicho pia kimeharibu zaidi ya dozi elfu 4 za kinga ya virusi vya corona na kuvunja hospitali 141 na kliniki ambapo ni 30 tu zilioanza kutoa huduma kamili.