1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Watu waliokufa kwa tetemeko Uturuki na Syria yafikia 9,000

8 Februari 2023

Vikosi vya uokozi nchini Uturuki na Syria wanaendelea kufanya kazi usiku na mchana na kuiondoa miili zaidi kutoka kwenye vifusi vya maelfu ya majengo yaliyoporomoka kutokana na tetemeko kubwa la ardhi.

https://p.dw.com/p/4NDsM
Syrien Erdbeben Rettungsarbeiten Aleppo
Picha: BAKR ALKASEM/AFP

Idadi ya vifo imepanda leo na mpaka sasa inakaribia watu 10,000, na kulifanya tetemeko hilo kuwa baya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika zaidi ya muongo mmoja.

Shirika la kushughulikia majanga la Uturuki limesema idadi ya vifo nchini humo imepanfa hadi 6,957, na kufikisha jumla ya watu 9,600, wakiwemo waliokufa katika nchi jirani Syria tangu janga hilo la Jumatatu na matetemeko mengine madogo yaliyofuata.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Syria, idadi ya waliokufa katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali imepanda hadi watu 1,250 huku 2,054 wakijeruhiwa. Karibu watu 1,280 wamekufa katika maeneo ya kaskazini magharibi yanayodhibitiwa na waasi.