1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu watano wafariki baada ya kuvuta gesi ya metani, Congo

15 Februari 2023

Hofu imetanda katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bulengo mjini Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya watu watano kufariki, vifo vyao vikiaminika kusababishwa na kuvuta gesi ya metani.

https://p.dw.com/p/4NV3X
Kongo I Kanyaruchinya Lager für Binnenvertriebene
Picha: Guerchom Ndebo/AFP

Miongoni mwa maelfu ya watu waliokimbia mapigano kati ya jeshi la congo na waasi wa M23 wiki mbili zilizo pita  nakuja kupata hifadhi kwenye kambi hii, ambayo mazingira yake sasa yamekuwa tishio kubwa kwa maisha yao, kutokana na uwepo wakiwango cha juu cha gesi ya metani inayoweza kusababisha kifo.

Mapigano makali yazuka kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23

Mabinti Yalala na Mafuluko wote wakiwa ni kutoka familia moja, wamebaki bila mzazi baada yakumpoteza baba aliyekufa kutokana na madhara yatokanayo na kupumua gesi hiyo.

Sehemu zote ndani ya kambi hii inayo pakana na ziwa kivu  ambalo lina hazina kubwa ya aina hiyo yaa gesi, hofu imeongezeka kwa wakimbizi hao wa ndani ambao baadhi ni wanawake na watoto walio tengana na familia zao wakati wamapigano kwenye mji wa kitshanga  huko wilayani masisi.

Ukosefu wa usalama Goma wafanya hali kuwa ngumu zaidi

FILE PHOTO: Congo rebels seize key border town
Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mjini GomaPicha: Djaffar Sabiti/REUTERS

Imekadiriwa kuwa zaidi ya watu elfu mbili wamepata hifadhi kwenye Kambi hii ya bulengo iliyotengwa na serikali ya congo lakini hadi sasa haina alama zinazoonyesha maeneo ya hatari na maelekezo kwa wakaazi wa kambi hiyo kuyaepuka maeneo hayo.

Hata hivyo, akizungumza na DW, Dedeci Mitima afisa wa serikali kwenye eneo hilo ambaye amethibitisha vifo vya watu ikiwemo kiongozi wa idara ya serikali kwa ajili ya usalama wa raia aliye poteza maisha yake mwishoni mwa wiki iliyopita.

DR:Congo: Waasi wa M23 wakabidhi kambi ya kijeshi ya Rumangabo, mashariki ya Kongo

Wakati gesi inaendelea kuongezeka katika ziwa Kivu, ongezeko hilo linakwenda sambamba na kitisho kwa maisha ya watu, na wakimbizi katika kambi ya Bulengo wanajikuta katika hatari kubwa zaidi hasa wakati huu wa vita.

Mwandishi: Benjamin Kasembe/DW Goma