1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watzke: Kibarua cha Favre kiko salama Dortmund

Deo Kaji Makomba
27 Mei 2020

Kocha wa Borussia Dortmund Lucien Favre ameungwa mkono na mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Hans-Joachim Watzke Jumatano. (26.05.2020). Bayern Munich iliishinda Dortmund 1-0 Signal Iduna Park.

https://p.dw.com/p/3cra5
Bundesliga VfL Wolfsburg - Borussia Dortmund Dortmunds Trainer Lucien Favre
Picha: picture-alliance/dpa/M. Sohn

"Nadhani Lucien amekuwa makini sana katika wiki zilizopita," alisema Watzke. "Haonekani kama mtu anayekabiliwa na shinikizo," aliongeza kusema.

Favre alisema baada ya kushindwa Jumanne angezungumza kuhusu hali Drtmund katika wiki chache zijazo, huku baadhi ya vyombo vya habari vikitafsiri kama kidokezo cha uwezekano wa kuondoka kabla mkataba wake kukamilika 2021.

"Sifikirii kuhusu kukata tamaa. Nilichotaka kukisema ni kwamba huu sio wakati wa kufanya tathmini," Favre aliliambia gazeti la WAZ siku ya Jumatano. "Tuna mechi sita kucheza na tunataka kufanya bidii kadri ya uwezo wetu."

Ushindi wa bao 1-0 iliyoupata timu ya Bayern Munich dhidi ya timu ya Borussia Dortmund iliyoko katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya kandanda ya Bundesliga umewafanya vinara wa ligi hiyo Bayern Munich kuendelea kujikita kileleni kwa tofauti ya alama saba na michezo sita mkononi dhidi ya wapinzani wao wa karibu Borussia Dortmund.
Bayern Munich kwa hivi sasa ina matumaini ya kunyakua taji la nane la ligi kuu ya Bundesliga baada ya ushindi wa bao 1-0 iliyoupata Jumanne 26.05.2020, dhidi ya wapinzani wao wa karibu Borussia Dortmund.

Tofauti kati ya Bayern chini ya kocha wa zamani Niko Kovac na sasa chini ya Hansi Flick ilionekana katika mchezo mzuri na wa kujiamini katika ushindi wa bao 1-0, licha ya kutokuwepo na mashabiki uwanjani kulikosababishwa na kuzuka kwa mlipuko wa virusi vya Corona.

Lilikuwa pambano la kusisimua, sio kama mashabiki walivyohofia halingewapa burudani. Kitu kilichojitokeza wazi ni jinsi Bayern walivyocheza mchezo wao, wakilikabili wimbi la mapema la Dortmund na baadaye kutumia ubunifu na kufunga bao.
Kupatikana kwa alama ingekuwa matokeo mazuri kwa Flick lakini timu yake ilishinda michezo 12 kati ya michezo yao 13 ya mwisho ya ligi na alijua ushindi utakuwa ni tumaini la ubingwa.
Mshambuliaji Joshua Kimmich, anaonekana kuwa mchezaji hodari ambaye anaweza kucheza katika nafasi yoyote uwanjani. Katika siku za usoni anatarajia kuwa nahodha wa Bayern na timu ya taifa ya Ujerumani. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 awali alionekana kuwa sio mtu mwenye nguvu na bidii.

Goli la Kimmich lawa gumzo

Shuti lake la ajabu kunako dakika 43, lilimvuka kwa juu mlinda mlango wa Borussia Dortmund liliwafanya mashabiki wote wa kandanda kukumbuka kwanini wanapenda mchezo wa soka na ni wangapi wameukosa wakati huu wa mlipuko janga la virusi vya Korona.

Goli hilo litakuwa ni miongoni mwa magoli ya kukumbukwa katika msimu huu na mipango ya awali kujaribu kumvuta  Roman Buerki kutoka kwenye mstari wake, ilionyesha kuwa Bayern sasa wamefanyia mazoezi kitu ambacho walishutumiwa kwa kutofanya wakiwa chini ya Kocha Kovac.

"Itakuwa ngumu kiakili kwa Dortmund kuendelea. Tunatakiwa kuhakikisha tena mwendelezo huu katika michezo inayofuata. Unaweza kuona kuwa ilikuwa ngumu sana na tulilazimika kufanya mazoezi hadi kuzifikia alama tatu," alisema Kimmich.

Flick alishinda 4-0 nyumbani dhidi ya Dortmund katika mchezo wake wa kwanza uliochezwa mnamo Novemba lakini ukilinganisha bado ifanisi wake ni madhubuti katika pambano hili ilikuwa ushahidi tosha kuonyesha ukomavu wake kama Kocha.

Erling Braut Haaland mwenye umri wa miaka 19 na Jadon Sancho waliotokea benchi kuongeza nguvu, haikushangaza kuona kwamba Dortmund hawawezi kuhimili ukomavu wa Bayern.

"Kiwango chetu kwa ujumla kilikuwa sawa, haswa mwanzoni mwa nusu ya kwanza na katika nusu ya pili. Lakini kuna mambo kadhaa yalikosekana; usahihi, harakati sahihi, mipira michache ya mwisho, kuongeza kasi na mpira na mashuti zaidi kuelekea lango la wapinzani,"alisema kocha Lucien Favre. "Hatupaswi kusahau kuwa tulicheza dhidi ya timu nzuri sana. Bayern inatetea vizuri sana na imejipanga vizuri."

Bundesliga Borussia Dortmund v FC Bayern München Kimmich
Joshua Kimmich akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao dakika ya 43Picha: Getty Images/F. Gambarini


Uamuzi wake wa kumfuta Mario Goetze na kuzingatia wachezaji wachanga inasikika lakini kwa busara na kihemko mashabiki wengi wangesema hawezi kujilinganisha na Juergen Klopp, mtu wa mwisho kushinda taji na Dortmund. Dortmund inaweza kuwa na mlima wa kupanda hata kama Bayern kwa namna fulani itateleza katika wiki zijazo.

Kocha wa Augsburg Heiko Herrlich alilalama wiki hii kuwa Ujerumani imechoshwa kuona Bayern kama mabingwa.


Na Deo Kaji Makomba/dpa/reuters