Waumini wa Orthodox Ethiopia washerehekea Krismasi
8 Januari 2025Waumini wa dini ya kikristo wa madhehebu ya Orthodox nchini Ethiopia walisherekea sikukuu ya Krismasi siku ya Jumanne kwa maombi ya amani kwa taifa hilo la pembe ya Afrika wakati taifa hilo likikabiliwa na migogoro mikubwa katika miaka ya hivi karibuni.
Waethiopia wanafuata kalenda ya Julian, ambayo iko mbele siku 13 kwa kalenda ya Gregoria, inayotumiwa na makanisa ya Kikatoliki na Kiprotestanti. Waethiopia wanasherehekea sikukuu hiyo kwa kuchinja wanyama na kuwakutanisha wanafamilia kwa chakula cha pamoja. Wakristo Ethiopia wamlaumu Abiy kushindwa kuzuwia mauaji
Sherehe hiyo inafanyika siku chache baada ya taifa hilo kukumbwa na majanga ya asili ikiwa ni pamoja na maporomoko ya ardhi yaliyowaacha maelfu ya watu bila makaazi katika maeneo ya Afar, Amhara na Oromia.