1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMarekani

Wazima moto wapambana kuzuia moto mkubwa Los Angeles

13 Januari 2025

Maelfu ya watu waliolazimika kuondoka katika makaazi yao kutokana na moto mkubwa mjini Los Angeles, Marekani hawatarejea kwenye makaazi yao kwa angalau siku nne zijazo.

https://p.dw.com/p/4p5Ix
USA Los Angeles 2025 | Waldbrände in Mandeville Canyon
Moto ukiteketea katika eneo la Mandeville Canyon, Los AngelesPicha: Lokman Vural Elibol/Anadolu/picture alliance

Mkuu wa kikosi cha zima moto wa Los Angeles Anthony Marrone amesema upepo mkali unaovuma katika eneo hilo, kunamaanisha kwamba bado eneo hilo liko chini ya hali ya tahadhari.

Mkuu huyo wa kikosi cha zima moto ameongeza kuwa, kwa wakati huu sio salama kwa watu kurudi kwenye makaazi yao.

Soma pia: Trump awakosoa viongozi wa California wanavyoshughulikia janga la moto 

Wazima moto wanaendelea kuudhibiti moto mkali ambao umesababisha vifo vya watu 24 huku wengine 16 hawajulikani waliko.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa imetahadharisha juu ya kutokea kwa upepo mkali wiki hii ambao huenda ukachochea kuenea kwa moto huo.