Waziri Blinken afanya mazungumzo kwa siku ya pili Beijing
19 Juni 2023Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anakamilisha hii leo ziara yake nchini China na amediriki siku ya pili na ya mwisho ya mikutano muhimu na maafisa wakuu wa Beijing, katika dhamira ya kupunguza mvutano inayoongezeka kati ya Marekani na China.
Mataifa hayo mawili yamedhihirisha nia ya kuendelea na mazungumzo licha ya kushindwa kuafikiana kuhusu masuala muhimu yanayopelekea kuongezeka kwa mivutano.
Soma pia: Blinken awasili China kupunguza joto la mivutano
Miongoni mwa mambo hayo ni masuala ya biashara, mzozo wa Taiwan, haki za binaadamu nchini China na Hong Kong pamoja na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Blinken alikutana na mwanadiplomasia mkuu wa China Wang Yi kwa takriban saa tatu, na atakutana na Rais Xi Jinping kabla ya kuondoka leo jioni.
AP