Waziri Lwin wa Myanmar azuwiwa kushiriki mkutano wa ASEAN
3 Februari 2022Matangazo
Hatua hii imechukuliwa baada ya tathimini ya utekekelezaji wa mapendekezo yaliokubaliwa na viongozi mwaka jana, kujaribu kutuliza mzozo unaoikumbwa Myanmar.
Cambodia ambayo inashikilia uwenyekiti wa jumuiya ya ASEAN, imesema kutokana na kutokuwepo maendeleo katika utekelezaji wa muafaka huo, mataifa wanachama hawakuafikiana juu ya kumualika waziri wa mambo ya nje wa Myanmar Wunna Maung Lwin kushirika mkutano ujao wa mawaziri wa mambo ya nje.
soma zaidi: Vifo zaidi vya waandamanaji vyaripotiwa Myanmar
Hatua hiyo imekuja siku 10 baada ya jumuiya ya ASEAN yenye wanachama 10 kuchukuwa hatua isiyo kifani kwa kumuzuwia kiongozi wa kijeshi wa Myanmar Min Aung Hlaing, kuhudhuria mkutano wa kilele mwezi Oktoba mwaka jana.