1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu mpya wa Haiti ahidi uchaguzi wa haraka

29 Julai 2021

Waziri Mkuu mpya wa Haiti, Ariel Henry amefanya ameahidi kufanyika uchaguzi wa haraka wa taifa hilo, kufuatia kuuwawa kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Jovenel Moise huku bado kukiwa na vurugu za maandamano ya wananchi.

https://p.dw.com/p/3yDmG
Haiti I  Ariel Henry wird Premierminister
Picha: Matias Delacroix/AP/picture alliance

Waziri Mkuu mpya wa Haiti, Ariel Henry amefanya ameahidi kufanyika uchaguzi wa haraka wa taifa hilo, kufuatia kuuwawa kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Jovenel Moise huku bado kukiwa na vurugu za maandamano ya wananchi ya ya kupinga mataifa ya kigeni kuingilia siasa za ndani. 

Henry amesema mpango wa serikali yake ni kufanikisha uchaguzi huru, wa kuaminika, wenye uwazi ambao utawashirikisha wapiga kura wengi huku akisisitiza hitaji la usalama nchini humo. Lakini pia amezungumzia takwa la kukabiliana na tatizo la ajira na kuujengea uwezo mfumo wa kimahakama wa nchi hiyo na kuongheza amekutana na viongozi wa asasi za kiraia tangu ale kiapo chake Julai 20. Zaidi alisema "Majadiliano hadi wakati huu bado magumu lakini yenye tija. Mazungumzo yanatoa umuhimu wa maridhiano kwa taifa la Haiti." Alisema kiongozi huyo mpya.

Ariel Henry atoa pendekezo la muundo mpya wa serikali ya Haiti

Haiti I  Ariel Henry wird Premierminister
Picha: Joseph Odelyn/AP/picture alliance

Pasipo kutoa ufafanuzi zaidi na wala kutoa fursa ya maswali mbele ya waandishi wa habari waziri mkuu huyo alisema alisisita umoja na kuongeza kwamba angalipenda muundo mpya wa serikali, ambao utakuwa na uwazi na pamoja na yote usizongwe na rushwa.

Mkutano huo ambao umedumu kwa takribani dakika 10, umefanyika katika kipindi cha tofauti ya masaa machache baada ya Henry kukutana na baraza la mawaziri katika mkutano wa ndani. Katika mkutano huo, inatajwa kwamba alitoa taarifa ya maendeleo ya uchunguzi wa mauwaji ya Julai, 7 ya Rais Moise. Kiongozi huyo aliwawa akiwa katika makazi yake binafsi kwenye mkasa ambao pia mke wake alijeruhiwa vibaya.

Watuhumiwa 28 watiwa mbaroni kwa tuhuma za mauwaji ya Rais Moise

Takribani watu 28 wametiwa mbaroni kutokana na tuhumza na mauwaji hayo, wakewomo wanajeshi 18 wa zamani wa Colombia, pamoja na afisa wa ngazi ya juu wa polisi ambae alikuwa akiongoza timu ya usalama wa rais Moise. Lakini bado serikali inaendelea kuwasa watuhumiwa wengine akiwemo, kiongozi wa waasi wa zamani, seneta wa zamani wa Haiti pamoja na jaji wa Mahakama Kuu wa Haiti.

Wakati huohuo idadi kadhaa ya watu kutoka katika makundi ya upinzani yalifanya maandamano katika mji wa Poirt au Prince ya kupinga kile walichosema mataifa ya kigeni kuingilia masuala ya ndani ya Haiti. Katika maandamano hayo waandamaji pamoja na kuchoma matairi moto walibeba mabango mbalimbali ya yenye kuonesha kuwa mataifa ya kigeni kama Marekani hayana upendo nao.

Hayo yanatokea wakati taifa hilo likiwa linaadhimisha miaka 218 tangu kufanyika kwa uvamizi wa Marekani kwa taifa hilo la kisiwa.

Chanzo: AP