1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu Starmer aapa kuwawajibisha wahusika wa ghasia

5 Agosti 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amewaonya waandamanaji wa siasa kali kuwa watajutia kushiriki katika ghasia mbaya zaidi nchini humo katika kipindi cha miaka 13.

https://p.dw.com/p/4j6dy
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir StarmerPicha: Benjamin Cremel/AP/picture alliance

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amewaonya waandamanaji wa siasa kali kuwa watajutia kushiriki katika ghasia mbaya zaidi nchini humo katika kipindi cha miaka 13. Kauli hiyo ameitoa kufuatia machafukoyanayohusishwa na mauaji ya watoto watatu mapema wiki hii yakizidi kupamba moto kote nchini.

Waandamanaji waliojifunika nyuso zao wanaopinga wahamiaji, walivunja madirisha kadhaa katika hoteli ambayo imekuwa ikitumika kuwahifadhi watu wanaotafuta hifadhi katika mji wa Rotherham.

Machafuko hayo yanayohusiana na taarifa za uongo kuhusu mauaji ya watu wengi Jumatatu iliyopita katika mji wa Southport ulioko kaskazini magharibi mwa Uingereza yameenea katika miji mingi, huku waandamanaji wanaopinga wahamiaji wakipambana na polisi.

Wazri Mkuu Starmer ameapa kuwashughulikia moja kwa moja wale walioshiriki ghasia hizo. Ghasia hizo ndio changamoto kubwa kwa Starmer aliyechaguliwa mwezi mmoja uliopita.