1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Modi ataka Umoja wa Afrika kuwa mwanachama wa kudumu G20

27 Agosti 2023

Waziri mkuu wa India Narendra Modi ametoa mwito hii leo kwa Umoja wa Afrika kuwa mwanachama wa kundi la G20, huku akiitaja India kama suluhisho la matatizo ya ugavi kimataifa.

https://p.dw.com/p/4VciN
India imekuwa ikiupigia debe Umoja wa Afrika kuwa mwanachama wa kundi la G20
Waziri mkuu wa India Narendra Modi akiwa katika kongamano la kilele la kibiashara la B20 huko New Delhi.Picha: Sajjad Hussain/AFP

Amesema hayo kabla ya mkutano wa kilele wa Kundi la Mataifa Tajiri na yale yanayoinukia kiuchumi la G20, utakaofanyika mjini New Delhi mwezi ujao.

Modi ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo amesema kwenye kongamano la kibiashara la B20 kuelekea mkutano huo wa kilele kwamba wameukaribisha Umoja wa Afrika kwa lengo la kuupatia uanachama wa kudumu.

Soma Pia: Rais wa Senegal apigia upatu Umoja wa Afrika kujiunga G20

Umoja huo wenye wanachama hai 55, hata hivyo umewasimamisha wanachama wake watano wanaotawaliwa kijeshi kufuatia mapinduzi.