1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al-Sudani ataka kikosi cha Marekani kiondoke Irak

18 Januari 2024

Waziri Mkuu wa Irak Mohammed al-Sudani ameshinikiza kuondoka kwa muungano wa kikosi cha kimataifa kinachoongozwa na Marekani kupambana na wanamgambo wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu nchini humo.

https://p.dw.com/p/4bR2w
Mohammed Shia Al-Sudani
Waziri Mkuu wa Irak Mohammed Shia Al-SudaniPicha: Murtadha Al-Sudani/Anadolu Agency/Pool via REUTERS

Katika matamshi aliyoyatoa kupitia televisheni huko Davos, Uswisi, al-Sudani amesema dola la kiislamu kwa sasa si kitisho tena kwa Irak na kwamba majeshi ya nchi hiyo yamejiandaa vyema kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi.

Marekani yashambulia wanamgambo wanaoiunga mkono Iran

Muungano wa kikosi hicho kinachoongozwa na Marekani ulianzishwa baada ya kundi hilo la kigaidi kuyateka maeneo makubwa ya kaskazini mwa Irak na nchi jirani ya Syria mwaka 2014.

Mwaka 2017 lakini, Irak ilitangaza ushindi dhidi ya kundi hilo.