Waziri Mkuu wa Jordan, Bisher Khasawneh ajiuzulu
15 Septemba 2024Hayo ni kulingana na maafisa wenye ufahamu juu ya suala hilo. Mkuu wa Ofisi ya Mfalme Abdullah, Jaafar Hassan aliyewahi pia kuwa Waziri wa Mipango, anatarajiwa kushika nafasi ya Kasawneh. Waziri Mkuu Bisher Khasawneh, mkongwe wa diplomasia na mshauri wa zamani wa Mfalme, aliteuliwa miaka minne iliyopita.
Itakumbukwa kuwa Jumatano wiki hii, chama cha upinzani cha Kiislamu cha IAF nchini humo, ambacho ni tawi la chama cha Udugu wa Kiislamu, kilishinda viti 31 kati ya 138 katika uchaguzi wa bunge.
Soma zaidi: Chama cha Kiislamu chapata ushindi wa kihistoria uchaguzi wa bunge Jordan
Kulingana na matokeo rasmi, ushindi wa chama hicho cha Kiislamu ndiyo mkubwa zaidi tangu mwaka 1989 ambapo chama cha Udugu wa Kiislamu kilipata viti 22 kati ya 80 katika bunge la wakati huo.