Waziri mkuu wa Libnan awaonya wanamgambo wa kisuni wasalim amri au watakiona cha mtema kuni
27 Mei 2007Washington/Beirut:
Marekani imetuma vifaa zaidi vya kijeshi nchini Libnan ambako jeshi linapambana na wanaharakati wa kiislam waliojificha ndani ya kambi za wakimbizi wa kipalastina.Waziri mkuu wa Libnan Foaud Siniora amewatolea mwito kwa mara nyengine tena wanamgambo hao wa kisunni wasalim amri au wakabiliane na hujuma za jeshi la Libnan.Waziri mkuu Fouad Siniora amesema hayo baada ya mkuu wa wanamgambo wa kishiya Hisbollah,Sheikh Hassan Nasrallah kuonya pindi jeshi likiivamia kambi ya wakimbizi,basi wimbi jipya la matumizi ya nguvu litaripuka nchini Libnan.Mapigano ya siku sabaa kati ya wanaharakati wa kisunni wanaotajikana kua na mafungamano na kundi la magaidi la al Qaida na jeshi la Libnan yaligharimu maisha ya dazeni kadhaa ya watu.Maelfu wakazipa kisogo kambi za wakimbizi karibu na Tripoli huku watumishi wa mashirika ya kiutu wakijaribu kuwapatia misaada ya chakula na madawa maelfu wengine walioamua kusalia katika kambi hizo.