1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Christopher Luxon aomba msamaha kwa unyanyasaji wa umma

12 Novemba 2024

Waziri Mkuu wa New Zealand Christopher Luxon, ameomba msamaha rasmi katika bunge kwa unyanyasaji ulioenea, mateso na kutelekezwa kwa maelfu ya watoto katika nyumba za malezi, taasisi za umma na kidini.

https://p.dw.com/p/4musY
Waziri Mkuu wa New Zealand Christopher Luxon
Waziri Mkuu wa New Zealand aomba msamaha rasmi kwa unyanyasaji wa ummaPicha: Lawrence Smith/Stuff/picture alliance

Luxon amekiri kwamba vitendo vilivyofanyika vilikuwa vya kutisha, kuvunja moyo na havipaswi kutokea tena, wakati alipozungumza mbele ya bunge na kufuatiliwa na mamia ya manusura wa unyanyasaji. 

Takribani watu 200,000 katika taasisi za umma kama vile hospitali na shule, nyumba za malezi na zile za kidini walipitia unyanyasaji usiofikirika katika kipindi cha miongo saba.

Waziri Mkuu wa China aanza ziara nchini New Zealand

Hayo yalibainishwa katika ripoti ya kutisha iliyotolewa mwezi Julai katika uchunguzi mkubwa zaidi kuwahi kufanya nchini New Zealand. Unyanyasaji huo unatajwa kuwa wa kimwili, kingono na kisaikolojia.