SiasaPakistan
Pakistan kukutana kwa dharura baada ya kushambuliana na Iran
19 Januari 2024Matangazo
Waziri wa Habari wa Pakistan Murtaza Solangi amesema mkutano huo unafanyika baada ya nchi hizo mbili kushambuliana kwa droni na makombora.
Kwa mujibu wa Solangi, mkutano huo utajadili maslahi mapana ya usalama wa taifa baada ya mashambulizi kati ya Iran na Pakistani.
Umoja wa Mataifa na Marekani zimehimiza ustahimilivu na kujizuia, huku China ikijitolea kuwa mpatanishi katika mzozo huo.
Afisa wa usalama wa Pakistan amesema mkuu wa majeshi na mkuu wa idara za upelelezi watahudhuria mkutano huo.
Waziri Mkuu Kakar jana alikatisha ziara yake huko Davos, Uswisi alikokuwa anahudhuria mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani.