1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaThailand

Waziri Mkuu wa Thailand atangaza uchaguzi mkuu kufanyika Mei

21 Februari 2023

Waziri Mkuu anayekabiliwa na shinikizo nchini Thailand Prayut Chan-O-Cha ametangaza leo kuwa uchaguzi mkuu wa taifa hilo utafanyika mnamo mwezi Mei na tayari kampeni za awali zimekwishaanza.

https://p.dw.com/p/4NnfV
Thailand | Prayuth Chan-ocha
Picha: Sakchai Lalit/AP Photo/picture alliance

Chan-O-Cha ambaye yeye mwenyewe anawania uchaguzi huo licha ya ukosoaji unaoandama utawala wake, amesema atalivunja bunge mnamo mwezi Machi ili kufungua njia ya uchaguzi kufanyika mwezi Mei.

Katika wakati uchumi wa  Thailand umeterereka na sekta muhimu ya utalii imeathiriwa na janga la corona, uchaguzi huo utakuwa kipimo kwa utawala wa Chan-O-Cha ambaye umaarufu wake umeporomoka.

Kiongozi huyo atatetea kiti chake kupitia chama kipya alichokiunda cha Ruam Thai Sang baada ya chama tawala kusema kitampendekeza mwanasiasa mwengine kuwania kiti cha waziri mkuu.