1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe ajiuzulu

3 Julai 2020

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Edouard Philippe amejiuzulu huku mabadiliko ya serikali yakitarajiwa kufanyika katika siku zijazo.

https://p.dw.com/p/3ejPV
Frankreich, Le Havre I Wahl 2020 I Edouard Philippe
Picha: picture-alliance/R. Lafargue

Kulingana na Ikulu ya Elysee, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atamchagua waziri mkuu mpya katika muda wa saa chache zijazo.

Rais Emmanuel Macron anatarajia kuanza awamu mpya ya miaka miwili iliyobaki ya muhula wake wa uongozi. Macron anataka kuzingatia zaidi kuuinua uchumi wa Ufaransa uliodhoofishwa na janga la virusi vya corona.

Mabadiliko hayo yanafanyika kufuatia uchaguzi wa manispaa wa Jumapili iliyopita, ambapo chama cha Kijani kilikishinda chama cha Macron katika miji mikubwa nchini humo.

Mabadiliko hayo yalipangwa kabla ya kufanyika uchaguzi, kwani serikali ya Macron imekuwa ikikosolewa wakati wa janga la virusi vya corona.