1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiPakistan

Waziri Mkuu wa zamani Pakistan ahukumiwa miaka 10 jela

30 Januari 2024

Mahakama moja nchini Pakistani leo imemhukumu waziri mkuu wa zamani Imran Khan na moja ya manaibu wake kifungo cha miaka 10 jela kila mmoja, baada ya kutiwa hatiani kwa kuvujisha siri za serikali.

https://p.dw.com/p/4bqAJ
Lahore, Pakistan | Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan
Waziri Mkuu wa zamani Pakistan Imran KhanPicha: Akhtar Soomro/REUTERS

Hukumu hiyo ni pigo jingine kwa Khan, mchezaji mashuhuri wa zamani wa kriketi aliyegeukia siasa, ambaye aliondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani bungeni mnamo Aprili 2022. 

Kulingana na msemaji wa chama cha Khan cha  Tehreek- e-Insafhukumu hiyo imetolewa na mahakama ya mji wa Rawalpindi chini ya ulinzi mkali wa polisi. 

Soma pia:Imran Khan ahukumiwa kwenda jela miaka 10

Mamlaka za nchi hiyo zimesema Khan ambaye sasa anatumikia kifungo kingine cha miaka 3gerezani kwa makosa ya rushwa anayo haki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo ya leo.

Mara kadhaa mwanasiasa huyo amesema kesi zote zinazomkabili zimechochewa kisiasa.