Nawaz Sharif arejea Pakistan baada ya miaka minne uhamishoni
21 Oktoba 2023Sharif anarejea nyumbani kuelekea uchaguzi mkuu katika taifa hilo unaotarajiwa kufanyika mwezi Januari mwakani, ambapo anatafuta kupata uungwaji mkono wa wapiga kura. Akiwahutubia waandishi wa habari kabla ya kuondoka Dubai kuelekea Islamabad, Sharif amesema kuwa leo anaelekea Pakistan baada ya miaka minne na anaona raha sana kwa neema ya mwenyezi Mungu.
Soma pia: Pakistan yamruhusu Sharif kurejea nyumbani kutoka uhamishoni
Sharif ameonPakistan yamruhusu Sharif kurejea nyumbani kutoka uhamishonigeza kuwa anatamani hali nchini Pakistan ingekuwa imeimarika wakati alipokuwa uhamishoni alipokimbilia mnamo mwaka 2019 miaka miwili baada ya kujiuzulu wadhifa wa waziri mkuu baada ya kutiwa hatiani kwenye kesi ya ufisadi. Sharif atasafiri kuelekea mji mkubwa wa Mashariki wa Lahore, ambapo wafuasi wake tayari wamekusanyika kwa ajili ya mkutano wa kumkaribisha.