Suella Braverman atarajiwa kufanya ziara nchini Marekani
24 Septemba 2023Braverman anatarajiwa kuwasilisha muongozo kuhusu jinsi mataifa yanaweza kukabiliana na mzozo wa uhamiaji haramu na kuangazia jinsi Uingereza imekuwa kinara katika kuleta mbinu za ubunifu kushughulikia suala hilo.
Soma pia:EU agency agrees to help Athens deport more migrants
Braverman amesema uhamiaji haramu na harakati za kuhama kwa watu wengi kote ulimwenguni ambazo hazijawahi kutokea, zinaweka shinikizo kali kwa Marekani, Uingereza na Ulaya.
Braverman kufanya mazungumzo na maafisa wakuu wa Marekani
Braverman, ambaye atasafiri kuelekea Marekani kesho Jumatatu, atatafuta ushirikiano wa karibu na nchi hiyo katika kushughulikia uhamiaji haramu na uhalifu wa vikundi vya kuratibu uhamiaji. Katika ziara hiyo, Braveman atafanya mazungumzo na wabunge pamoja na maafisa wakuu wa Marekani.