1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Choe Son Hui, kufanya ziara fupi Urusi

29 Oktoba 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini, Choe Son Hui, anatarajiwa kuwasili mjini Moscow, kufanya ziara ya pili nchini Urusi katika kipindi cha wiki sita.

https://p.dw.com/p/4mL55
Choe Son Hui I Korea Kaskazini
Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini, Choe Son HuiPicha: Luong Thai Linh/AFP/Getty Images

Waziri Choe Son anafanya ziara hiyo katika muktadha wa tuhuma juu ya nchi yake kutaka kuingia katika vita vya Urusi na Ukraine.

Jumuiya ya kijeshi ya NATO, Korea Kusini na Marekani zimeungana katika kuthibitisha kuwa Korea Kaskazini imepeleka wanajeshi nchini Urusi.

NATO imesema vikosi vya jeshi la Korea Kaskazini vilipelekwa katika eneo la Urusi la Kursk kwenye mpaka na Ukraine. 

Waziri wa Mambo ya nje wa Korea Kaskazini azuru Moscow

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema Marekani haitaweka vizuizi vipya kwa Ukraine kutumia silaha za Marekani ikiwa Korea Kaskazini itaingia katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine. 

Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, inadai kuwa Korea Kaskazini imepeleka askari 10,000 mashariki mwa Urusi kwa ajili ya mafunzo.