1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kusafiri kwenda China

10 Juni 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken atasafiri kuelekea China wiki ijayo kwa ajili ya mazungumzo ya muda mrefu yaliyocheleweshwa.

https://p.dw.com/p/4SPrh
Norwegen | Antony Blinken NATO Außenministertreffen in Oslo
Picha: Hanna Johre/NTB/REUTERS

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken atasafiri kuelekea China wiki ijayo kwa mazungumzo ya muda mrefu yaliyocheleweshwa yenye lengo la kupunguza msuguano baina ya nchi hizo mbili.

Afisa mmoja wa Marekani ameeleza kuwa Blinken anatarajiwa kuwasili Beijing mnamo Juni 18 japo hakutoa maelezo zaidi.

Shirika la habari la Reuters siku ya Jumatano liliripoti kuwa mwanadiplomasia huyo wa Marekani atasafiri kwenda China wiki zijazo, likinukuu vyanzo ambavyo vilizungumza kwa sharti la kutotajwa jina.

Mnamo mwezi Februari, Blinken aliifuta ziara ya Beijing aliyoipanga ambayo ingekuwa ya kwanza kufanywa na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani katika muda wa miaka mitano, juu ya madai ya China kutuma puto za kijasusi katika anga ya Marekani.