1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waziri wa mambo ya nje wa Thailand akutana na Suu Kyi

12 Julai 2023

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Thailand Don Pramudwinai amesema amekutana na kiongozi wa zamani wa Myanmar aliye gerezani Aung San Suu Kyi,

https://p.dw.com/p/4TmZC
Aung San Suu Kyi
Picha: Ann Wang/REUTERS

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Thailand Don Pramudwinai amesema amekutana na kiongozi wa zamani wa Myanmar aliye gerezani Aung San Suu Kyi, akiwa afisa wa kwanza wa kigeni kuruhusiwa kuonana na mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel tangu alipowekwa kizuizini na utawala wa kijeshi miaka miwili iliyopita.

Mwanadiplomasia huyo ameyasema hayo alipozungumza na waandishi habari pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa Kundi la Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN, unafanyika nchini Indonesia.

Pramudwinai amesema alikutana na Suu Kyi siku ya Jumapili na walizungumza kwa muda wa saa moja na nusu na kwamba afya yake nzuri. Amearifu kwamba wakati wa mkutao huo Suu Kyi alizungumzia uungaji wake mkono kwa mazungumzo yanayoendelea katika juhudi za kuumaliza mzozo wa kisiasa nchini Mynamar ulizuka baada ya jeshi kufanya mapinduzi mwaka 2021.