Waziri wa Ulinzi Ujerumani aanza ziara, Mataifa ya Baltic
25 Septemba 2023Matangazo
Pistorius akiambatana na ujumbe wake, anatarajia kufanya mazungumzo kuhusu hali jumla ya usalama na ushirikiano zaidi wa kijeshi na Latvia ambayo pia ni mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami NATO.
Kesho Jumanne, Ujumbe wa Ujerumani utaelekea Estonia kunakotarajiwa Mkutano wa kila mwaka wa ulinzi wa kanda hiyo ya Baltic. Ujerumani imezidisha kwa kiasi kikubwa ushiriki wake wa kijeshi katika Mataifa ya Baltic baada ya Urusi kuanzisha vita vyake dhidi ya Ukraine.
Berlin imekua ikishirikiana mno na Lithuania na inapanga katika siku za usoni kutuma nchini humo kikosi kitakachokuwa tayari kwa mapambano.