1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Waziri wa ulinzi wa Israel aliyefutwa kazi ajiuzulu bungeni

2 Januari 2025

Waziri wa zamani wa ulinzi nchini Israel, Yoav Gallant, aliyeondolewa mwezi Novemba baada ya kuongoza kampeni ya kijeshi dhidi ya Ukanda wa Gaza kwa zaidi ya mwaka mmoja, ametangaza kujiuzulu ubunge.

https://p.dw.com/p/4okks
Israel | Yoav Gallant | IDF
Waziri wa zamani wa ulinzi nchini Israel, Yoav Gallant.Picha: DREW ANGERER/AFP/Getty Images

Galant tayari ameshawasilisha barua yake ya kujiondoa bungeni kwa spika wa bunge la Israel. 

Amesema baada ya kuitumikia jeshi la IDF kwa miaka 35 na muongo mzima katika serikali na bunge ni wakati sasa wa kuangalia mwelekeo mwengine.

"Kama ilivyo katika uwanja wa mapambano ndiovyo ilivyo katika huduma ya umma. Kuna wakati ambapo mtu lazima aache anachokifanya, aangalie upya na kuchukua muelekeo mwengine ili kufikia malengo yanayohitajika Njia ya Likud ndio njia yangu naamini kanuni zake na naamini wanachama wake na wapiga kura. Kama waziri wa zamani wa ulinzi nawajibika kwa kila kitu kilichotokea mwanzoni mwa kazi yangu miezi kadhaa kabla ya kita na hadi mwisho wa kazi yangu zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuanza kwa vita."

Soma pia:  ICC yatoa waranti ya kukamatwa Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alimfuta kazi Galant akisema hakuna uaminifu baada ya kutokubaliana katika masuala kadhaa likiwemo la kuingizwa jeshini kwa waumini wa Kiyahudi wa madhehebu ya Orthodox, hatua iliyopingwa na Netanyahu akihofia linaweza kuivunja serikali yake inayotegemea nguvu za vyama vya kidini. 

Mwezi Novemba, Mahakama ya ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, ilitoa waranti ya kukamatwa Netanyahu, Gallant na kamanda wa kundi la Hamas, Mohammed Dief, kufuatia madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita kwenye Ukanda wa Gaza.