1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin taabani hospitali

12 Februari 2024

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin yuko wodi ya wagonjwa mahututi akiwa na tatizo la kibofu cha mkojo baada ya kuhamisha majukumu yake kwa naibu wake Jumapili, alipokuwa akipambana na saratani ya tezi dume.

https://p.dw.com/p/4cIT1
Lloyd Austin | Waziri wa Ulinzi wa Marekani
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd AustinPicha: Susan Walsh/AP/dpa/picture alliance

Naibu waziri wa ulinzi nchini Marekani Kathleen Hicks amekaimu majukumu ya Waziri wa ulinzi, Lloyd Austin aliyelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi akitibiwa matatizo ya kibofu cha mkojo wakati akikabiliwa pia na maradhi ya saratani ya tezi dume.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Pat Ryder kwenye taarifa amesema majukumu ya waziri Austin yamekabidhiwa kwa naibu wake jana Jumapili na kwamba ikulu na bunge zimearifiwa. Madaktari wanaomshughulikia wamesema yuko chini ya uangalizi wa karibu.

Wiki za hivi karibuni waziri huyo mwenye umri wa miaka 70 alilazwa hsopitali kwa siri bila ya kumuarifu rais Joe Biden kuhusu maradhi yake, hatua iliyoibuwa kauli za kumkosoa katika wakati ambapo Marekani inakabiliana na migogoro ya Mashariki ya kati na Ukraine.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW