Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin ziarani Cairo
8 Machi 2023Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema leo kuwa ushirikiano wa ulinzi wa Marekani na Misri ni nguzo muhimu ya dhamira ya Washington kwa Mashariki ya Kati. Austin ametoa kauli hiyo baada ya kutua mjini Cairo leo ikiwa ni kituo cha karibuni cha ziara yake ya Mashariki ya Kati. Anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi na maafisa wengine wa ngazi ya juu kabla ya kuondoka baadae leo kuelekea Israel. Waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Marekani amesema yuko Misri kuimarisha ushirikiano katika masuala muhimu.
Lloyd Austin yuko ziarani Mashariki ya Kati kujadili kitisho cha Iran kwa kanda nzimaMisri ni moja ya wapokeaji wakubwa katika Mashariki ya Kati wa msaada wa kiuchumi na kijeshi wa Marekani na mshirika wa dhati wa Marekani katika kanda hiyo. Lakini katika miaka ya karibuni, wabunge wa Marekani wameuwekea masharti msaada huo kutokana na masuala ya haki za binaadamu na mageuzi.