MigogoroSudan
Msaada wa nadra wa chakula wawasili Sudan
23 Agosti 2024Matangazo
Misaada hiyo imefanikiwa kuingia Sudan kupitia kivuko cha mpaka kilichofunguliwa kwa muda na Chad.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Stephane Dujarric, amesema zaidi ya malori kumi ya misaada yamevuka hadi Darfur kutoka Chad kupitia kivuko cha mpaka cha Adre.
Malori hayo ya shirika la WFP na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) yalikuwa yamebeba mtama, kunde, mafuta na mchele kwa ajili ya kuwasaidia takriban watu 13,000 wanaotishiwa na njaa katika eneo la Kereinik ,magharibi mwa Darfur.