1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Idadi ya wanaume wanaotumia tumbaku inapungua

19 Desemba 2019

Matumizi ya tumbaku miongoni mwa wanaume yameanza kupungua kwa mara ya kwanza, kulingana na ripoti ya kila mwaka ya shirika la afya duniani WHO.

https://p.dw.com/p/3V6LM
qualmende Zigarette in einer Hand
Picha: Imago Images/Sven Simon/F. Hoermann

Idadi ya wawanake wanaotumia tumbaku ilipungua kwa karibu milioni 100 kati ya mwaka 2000 hadi 2018. Hata hivyo, wanawake wameendelea kupunguza matumizi ya uraibu wa Nikotini ukilinganisha na wanaume.

Mwaka 2000, karibu theluthi tatu ya watu duniani walio na umri wa miaka 15 na zaidi walikuwa wakitumia tumbaku, sigara na bidhaa nyingine za tumbaku. Kwa ujumla idadi ya watumiaji tumbaku imepungua duniani kote, kutokana na serikali kuwa na sheria kali dhidi ya uraibu huo.

Kila mwaka watu zaidi ya milioni nane hupoteza maisha kutokana na athari za tumbaku ikiwemo watu milioni 1.2 ambao si wavutaji lakini wakiathirika na moshi wa wavutaji. Mataifa yaliyo na kiwango kikubwa cha uvutaji tumbaku ni yale ya Kusini mwa Asia Mashariki.