WHO: Kila taifa lisalie katika tahadhari ya hali ya juu
14 Mei 2020Hatua hiyo ilisababisha kudhibiti safari za raia wa kawaida na kuichagiza sekta ya utalii. Mataifa kadhaa ikiwemo Ujerumani, Austria na Uswisi zimetangaza mipango ya kulegeza masharti ya udhibiti wa mipakani kuazia katikati ya mwezi Juni, wakati bodi tendaji ya Umoja wa Ulaya ikitoa muongozo wa usalama katika kipindi cha kiangazi.
Kamishna wa Afya wa Umoja wa Ulaya, Stella Kyriakides amenukuliwa akisema raia wa Ulaya wanaweza kufanya safari za mapumziko au kwenda kuziona familia au marafiki katika miezi ya Juni hadi August, ingawa alionya pia kuwa lazima wajiweke katika tahadhari kwa kuwa safari hizo zinaweza kusababisha hatari za kupata maambukizi.
Dola bilioni 59.5 kuiondoa Italia katika mkwamo wa uchumi.
Kwengineko, Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte ametangaza uwasilishaji wa kitita cha dola bilioni 59.5 kwa ajili ya hatua ya kuanza ufufuzi wa uchumi na kuwasaidia wanachi katika taifa hilo ambalo ni miongoni mwa mataifa yaliotahiriwa vibaya kabisa na mripuko wa virusi vyacoronaduniani. Rekodi za sasa zinaonesha taifa hilo lina vifo 31,000. Na kwamba Umoja wa Ulaya umebashiri uchumu wa Italia utaporomoka kwa asilimia 9.5 kwa mwaka huu.
Marekani imeanza kaunzishwa upya uchumi wake baada ya miezi kadhaa ya mkwamo uliosababishwa na vizuizi vya kukabiliana na virusi vya corona, lakini wachambuzi wanasema itaweza kuchukua muda wa majuma kadhaa hadi kufahamika wazi kwamba, biashara zinazofunguliwa zitasababisha kupanga kwa maambukizi. Taifa hilo lina maambukizi zaidi ya watu milioni 1.4 na vifo zaidi ya elfu 80.
Brazil yarekodi vifo 749 kwa siku.
Wizara ya Afya ya Brazil imetoa takwimu zinazoonesha maambukizi mapya 11,385 ya virusi vya corona, pamoja na vifo 749 kwa siku. Hadi sasa taifa hilo lina idadi ya maambukizi 188,974, tangu kuanza kwa mripuko huko likiipita Ufaransa yenye maambukizi 177,700. Na kwa hali ilivyo nchini Brazil inabashiria kuwa taifa la sita litakaloathiriwa vikali duniani.
China imeripoti visa vitatu vya maambukizi ya virusi vya corona, ikiwa ni pungufu ya visa saba vilivyorekodiwa siku moja kabla. Wizara ya Afya ya China imesema visa vyote hivyo vimetokana na maambukizi ya ndani. Idadi ya maambukizi kwa sasa imefikia watu 82,929 wakati vifo vimesalia kuwa 4,633.
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika ya Kusini amesema ana lengo la kuendelea kuondosha vizuizi zaidi vilivyowekwa katika kukabiliana na janga la virusi vya corona lakini katika maeneo ambayo yameathiriwa zaidi, vitaendelea kuwepo hadi Juni. Kwa hatua hiyo Waafrika ya Kusini watashuhudia biashara zaidi zikifunguliwa na vyakula vikiuzwa.Taifa hilo lenye utajiri mkubwa kabisa wa kiviwanda barani Afrika limerekodi vifo 219 na maambukizi 12,074 hadi sasa.