1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yapoteza mawasiliano na wafanyakazi hospitalini ya Gaza

Angela Mdungu
25 Oktoba 2024

Shirika la afya duniani WHO, limesema kuwa limepoteza mawasiliano na wafanyakazi katika hospitali iliyosalia kaskazini mwa Gaza, baada ya jeshi la Israeli kudai kuwa limezingira eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4mF7A
Gazastreifen Indonesisches Krankenhaus Beit Lahia
Muonekano wa Hospitali ya Indonesia iliyoharibiwa huko Gaza City, Novemba 29, 2023.Picha: Mohammed Alaswad/AP/Zuma/picture alliance

Wizara ya afya ya Gaza ilisema mamia ya wagonjwa na wafanyakazi walikuwa wamezuiliwa katika hospitali ya Kamal Adwan. Wakati hayo yakijiri, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amekutana na mwenzake wa Jordan, Ayman Safadi, mjini London. Safadi ameishutumu Israel kwa kuhusika na mauaji ya kikabila huko Gaza."Njia pekee ya kuliokoa eneo hilo ni Israel kusimamisha hujuma dhidi ya Gaza na Lebanon, kusimamisha hatua za upande mmoja, hatua zisizo halali katika Ukingo wa Magharibi ambazo zinalitumbukiza eneo hilo shimoni".Safadi ni miongoni mwa viongozi wa nchi za Kiarabu waliokutana na Blinken kujadili usitishaji vita Gaza.