WHO yatala data za ugonjwa hatari wa kupumua
23 Novemba 2023Matangazo
WHO imefahamisha kwamba eneo la Kaskazini mwa China limeripoti ongezeko la maambukizi ya kile kinachoonekana kama homa ya mafua, tangu katikati ya mwezi Oktoba, ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita katika kipindi kama hicho. Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatano, shirika la afya duniani limeitaka China kutowa taarifa ya ufafanuzi zaidi kuhusu ongezeko la magonjwa ya kupumuwa pamoja na homa ya mapafu-Pneumonia kwa watoto.Wiki iliyopita tume ya kitaifa kuhusu masuala ya afya ya China iliwaambia waandishi habari kwamba kuongezeka kwa magonjwa hayo kumetokana na hatua ya kuondolewa vizingiti vya kuzuia kusambaa ugonjwa wa Uviko -19 pamoja na usambaaji wa virusi vinavyosababisha mafua na maambukizi ya bakteria.