JamiiItaly
Italia yatangaza tahadhari ya joto kali hii leo
19 Julai 2023Matangazo
Hali hiyo inashuhudiwa wakati wimbi la joto kali, moto wa nyika na mafuriko vikisababisha maafa kutoka Marekani hadi China. Wimbi la joto kali limeyakumba maeneo ya Ulaya ya Kusini wakati huu wa msimu wa majira ya joto ambao huvutia watalii, na kuvunja rekodi ikiwemo mjini Roma.
Mamlaka yatoa tahadhari ya kitisho cha vifo
Mabadiliko hayo yamesababisha mamlaka kutoa tahadhari ya ongezeko la kitisho cha vifo na mashinikizo ya moyo. Moto wa nyika umeshuhudiwa kwa siku ya tatu mfululizo magharibi mwa mji mkuu wa Ugiriki wa Athens, huku zoezi la kuuzima likiendelea mchana na usiku. Mjini Beijing, kiwango cha joto kimesalia juu ya nyuzi joto 35 kwa siku ya 28 mfululizo.