Wito wa vita kusitishwa Gaza kupisha chanjo ya polio
29 Agosti 2024Matangazo
Umoja huo umeungana na miito iliyotolewa na Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani, WHO, la usitishwaji wa mapigano ili kuruhusu maafisa wa afya kuwapa chanjo watoto.
Umoja wa Ulaya pia umepongeza utoaji wa zaidi ya dozi milioni 1.2 za chanjo za polio, pamoja na ushirikiano wa Israel katika kuzipeleka chanjo hizo Gaza.
Wakati huo huo, kiongozi wa upinzani wa Israel, Yair Lapid amekataa madai yaliyotolewa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwamba kiongozi wa Israel hakupokea onyo kuhusu shambulizi la Hamas.
Lapid ameliambia gazeti la Jerusalem Post kuwa Netanyahu alipewa taarifa, na yeye mwenyewe aliarifiwa, na taarifa hiyo ilitolewa kwa baraza la mawaziri.