Wito watolewa Haiti na Jamhuri ya Dominica kumaliza mvutano
19 Septemba 2023Afisa huyo, William O´Neill, anayeshughulikia masuala ya haki za bindamu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Haiti, amesema kufungwa mipaka ya nchi hizo kutaathiri ajira na biashara kwa raia wa pande mbili.
Pia ametahadharisha juu ya taathira kubwa katika upatikanaji wa bidhaa muhimu upande wa Haiti.
Jamhuri ya Dominica ilitangaza siku ya Ijumaa kuzifunga njia zote za mipaka na Haiti kupinga ujenzi wa mfereji utakaochepusha maji ya mto Massacre unaokatisha kwenye nchi hizo mbili.
Serikali ya nchi hiyo inasema ujenzi huo utaharibu mazingira na kutishia ustawi wa wakulima wa Jamhuri ya Dominica. Haiti kwa upande wake inasema inahitaji maji hayo ili kupunguza makali ya ukame kwenye wilaya yake ya Maribaroux.
O´Neill amezihimiza pande hizo mbili kutafuta suluhu kwa njia ya amani au ziombe usuluhishi wa kimataifa iwapo itahitajika.