1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wizara ya Afya Gaza yasema watu 38,664 wameuawa

15 Julai 2024

Wizara ya afya ya Ukanda wa Gaza inayoendeshwa na kundi la Hamas imesema takriban watu 38,664 wameuwawa katika vita kati ya Israel na wanamgambo wa kundi hilo la Palestina.

https://p.dw.com/p/4iJau
Hali kwenye Ukanda wa Gaza
Hali kwenye Ukanda wa Gaza.Picha: Mohammed Salem/REUTERS

Idadi hiyo imejumuisha vifo vipya vya watu 80 vilivyotokea ndani ya kipindi cha saa 24 zilizopita.

Taarifa ya wizara hiyo ya afya ya Gaza pia imeongeza kusema kwamba watu 89,097 wamejeruhiwa kwenye eneo hilo tangu vita vilipoanza Oktoba 7 baada ya wanamgambo wa Hamas kuishambulia Israel.

Kadhalika wizara hiyo imetoa takwimu mpya ya waliouwawa kufuatia mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya shule moja iliyoko katikati mwa Gaza yaliyofanyika jana Jumapili, inayoonesha waliouwawa wamefikia 22.

Shule hiyo ilikuwa ikisimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia wakimbizi Wakipalestina,UNRWA.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW