Xi, Biden wawasili Peru kwa mkutano wa kilele wa APEC
15 Novemba 2024Matangazo
Marais wa Marekani Joe Biden na Xi Jinping wa China wamewasili nchini Peru jana kwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia-Pasifiki APEC. Kuna uwezekano kwamba hiyo ndio itakuwa mara ya mwisho kwa Biden kukutana na Xi huku kukiwa na wingu la sintofahamu ya kidiplomasia kufuatia kuchaguliwa tena kwa Donald Trump. Huenda Biden akakutana na Xi Jinping
Biden na Xi wanatarajiwa kufanya mazungumzo siku ya Jumamosi, kando ya mkutano huo wa siku mbili. Jumuiya ya APEC, iliyoundwa mwaka wa 1989 kwa lengo la kukuza biashara huria ya kikanda, inazijumuisha nchi 21 ambazo kwa pamoja uchumi wake unawakilisha takriban asilimia 60 ya pato la taifa la dunia na zaidi ya asilimia 40 ya biashara ya kimataifa.