Rais Xi Jinping wa China akutana na viongozi wa Ulaya
7 Desemba 2023Matangazo
Rais wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, akiwa na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel na mkuu wa sera za nje wa Umoja huo Josep Borrell, wamesema zipo tofauti ambazo ni lazima zitatuliwe kati ya Umoja wa Ulaya na China, mshirika mkubwa wa kiuchumi wa Umoja wa Ulaya. China na Umoja wa Ulaya zimeongeza ushirikiano wa kidiplomasia mnamo mwaka huu, zikitaka kuharakisha kurekebisha uhusiano wao. Maafisa kadhaa wa Umoja wa Ulaya wameitembelea Beijing mara kwa mara ili kuanzisha upya mazungumzo ya ngazi ya juu.