Xi: Mataifa yenye nguvu fanikisheni amani Urusi na Ukraine
9 Julai 2024Mwito wa huo wa rais Xi umetolewa wakati wa ziara ya kiongozi wa Hungary mjini Beijing iliyotajwa na kiongozi huyo wa Umoja wa Ulaya, kama ziara ya ujumbe wa amani.
Ziara ya Orban China imefanyika siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa jumuiya ya kujihami ya NATO unaoanza leo huko Washington, ambako suala la Ukraine linatarajiwa kugubika mazungumzo ya viongozi wa jumuiya hiyo.
Soma pia:Waziri Mkuu wa Hungary , Rais Xi Jinping wakutana Beijing
Msemaji wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani John Kirby amesema Marekani ina wasiwasi na mkutano kati ya Orban na rais Xi kwasababu ziara hiyo haionekani ikileta tija katika kujaribu kutafutia ufumbuzi vita vya Ukraine.
China ni miongoni mwa nchi zilizokataa kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.