Xi, Putin waituhumu Marekani kuingilia nchi zao
8 Februari 2024Matangazo
Ikulu ya Kremlin imesema kuwa viongozi hao wawili wamefanya mazungumzo ya simu na kuilaani sera ya Marekani ya kutekeleza sera ya kuzidhibiti Urusi na China.
Nchi za Magharibi zinazitizama Moscow na Beijing, ambazo zinatafuta kutanua ushawishi wao wa kimataifa, kwa wasiwasi mkubwa katika miaka miwili iliyopita wakati zikiimarisha mahusiano yao katika biashara na ulinzi.
Moscow inaichukulia Beijing kama mshirika muhimu wa kiuchumi tangu Urusi ilivyowekewa vikwazo vikali na nchi za Magharibi kuhusiana na uvamizi wake wa kijeshi nchini Ukraine.
Nayo China imenufaika kutoka kwa bidhaa za bei nafuu za nishati ya Urusi, ikiwemo ununuzi wa gesi kupitia bomba la Power of Siberia.