1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Xi yuko safarini kuelekea Marekani kwa mkutano na rais Biden

14 Novemba 2023

Rais Xi Jinping wa China ameondoka mjini Beijing leo mchana kuelekea San Francisco kwa mkutano unaosubiriwa kwa shauku kati yake na rais Joe Biden wa Marekani siku ya Jumatano.

https://p.dw.com/p/4Yo2P
Indonesien G20 Joe Biden und Xi Jinping
Picha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

Rais Xi Jinping wa China ameondoka mjini Beijing leo mchana kuelekea San Francisco kwa mkutano unaosubiriwa kwa shauku kati yake na rais Joe Biden wa Marekani siku ya Jumatano.

Shirika la Utangazaji la China CCTV limeripoti kuwa Xi ameabiri ndege maalumu kuelekea Marekani kwa mwaliko wa rais Biden kwa mazungumzo muhimu yalifanikishwa kwa juhudi kubwa za kidoplamsia baina ya pande mbili.

Soma pia: APEC kuzingatia zaidi masuala ya usawa na mazingira

Viongozi hao wawili watafanya mazungumzo pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Nchi za Asia na Pasifiki, APEC, utakaofunguliwa kesho mjini San Francisco 

Huo utakuwa mkutano wao wa kwanza ndani ya mwaka huu uliotawaliwa na mivutano baina ya madola hayo mawili makubwa hususani kwenye masuala ya biashara, mzozo kuhusu vita vya Ukraine na hadhi ya kisiwa cha Taiwan.