YANGON : Kuna matumaini mazuri ya mazungumzo
8 Novemba 2007Matangazo
Njia imefunguliwa ya kuwepo kwa mazungumzo ya maana kati ya utawala wa kijeshi wa Myanmar na kiongozi wa upinzani anaeshikiliwa katika kifungo cha nyumbani Aung San Suu Kyi.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Myanmar amesema katika taarifa kwamba hivi sasa wana mchakato unaofanya kazi ambao utapeleka kufanyika kwa mazungumzo ya maana kati ya serikali na Suu Kyi kama hatua muhimu za kuleta usuluhishi wa kitaifa na kwa kuwajumuisha wahusika wote.
Gambari amesema hayo mwishoni mwa ziara yake ya siku sita nchini Myanmar ambapo leo alikutana tena na Suu Kyi baada ya kushindwa kuwashawishi viongozi wa kijeshi wahuhudhurie mkutano huo.